Serikali ya Tanzania inaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu  katika bandari ya Dar es Salaam ili kupunguza changamoto kubwa ya usafirishaji wa bidhaa ikiwemo matunda ya Parachichi kwa kupeleka bandari zilizopo nchi jirani.

Afisa mtendaji mkuu wa Tanzania Horticulture Association (TAHA) Dkt.Jacqueline Mkindi ameeleza hayo mkoani Njombe mara baada ya wawekezaji kueleza changamoto  hiyo ulipokuwa ukifanyika uzinduzi wa vituo vya kukusanyia mazao ya Horticulture mkoani humo.

"Kwa sasa hivi 80% ya kontena za Pachichi kwa hawa wasafirishaji bado zinapita Mombasa na unaona wawekezaji wako tayari kupita Mombasa na sio Dar kwanini ni kwasababu ya uwezo kuondokana na mambo mengine mengi lakini tunashukuru serikali kunamaendeleo makubwa yanafanyika Dar"

Amesema changamoto hizo zinakwenda kutatuliwa kwa kipindi kifupi kijacho kwasababu awali asilimia 100% wawekezaji walikuwa wakipita Mombasa na mabadiriko makubwa yameanza ambapo kuanzia mwaka 2021 asilimia 15% mpaka 20% ya kontena zinapita bandari ya Dar es Salaam.

Awali Meneja wa Avodemia, Mohamed Adam Jee ambao ni wawekezaji na wasafirishaji wa Parachichi,amesema kuwa uhitaji wa Parachichi za Tanzania huko Duniani ni mkubwa lakini wamekuwa wakipata shida na kutumia gharama kubwa kusafirisha zao hilo huku wakilazimika kutumia bandari ya Nje ya Tanzania kutokana na changamoto ya miundombinu iliyopo katika bandari ya Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt.Hussein Mohamed Omari amesema Serikali inafanyia kazi changamoto hizo ambapo pia Imeongeza bajeti Kwenye sekta ya kilimo kutoka Bilioni 294 hadi Trioni 1.28 na kwamba ujenzi wa vituo vya kupimia na kukusanyia Parachichi vilivyo jengwa na TAHA ni mkombozi kwa wakulima.

Jumla ya vituo vitano vya kukusanyia mazao ya horticulture vimezinduliwa mkoani Njombe ikiwa ni sehemu ya kuboresha miundombinu ili kupunguza upungufu wa upotevu wa mazao.






Share To:

Post A Comment: