Na MWANDISHI WETU,
TANGA. Waajiri wa sekta binafsi wametakiwa kuzingatia wajibu wao wa kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati ili kuwawezesha wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kupata mafao yao kwa mujibu wa sheria.
Wito huo umetolewa tarehe 8 Mei 2025 jijini Tanga na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Bi. Mwamini Malemi, wakati akizindua rasmi Mkutano wa 54 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mfuko huo.
Bi. Malemi amesema michango ya waajiri ni uti wa mgongo wa uendeshaji wa Mfuko, hivyo kucheleweshwa kwake kunaathiri moja kwa moja ustawi wa wanachama na ufanisi wa utoaji huduma za mafao.
“Naomba nitumie nafasi hii kuwaasa waajiri wote kuhakikisha wanawasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati. Hili si jambo la hiari bali ni wajibu wa kisheria unaolenga kulinda haki za wafanyakazi”, amesisitiza Bi. Malemi.
Ameongeza kuwa, NSSF inaendelea kutoa huduma bora na endelevu kwa wanachama wake kwa kuzingatia misingi ya uadilifu, uwajibikaji na matumizi ya teknolojia ili kuongeza uwazi na ufanisi katika shughuli za kila siku.
Akizungumza kuhusu mafanikio ya Mfuko, Bi. Malemi amesema NSSF imeendelea kuwa taasisi ya mfano katika sekta ya hifadhi ya jamii kwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA, kuongeza kasi ya uandikishaji wanachama, kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato na kufanya uwekezaji wenye tija.

“Lengo letu ni kuhakikisha kila mwanachama anaendelea kupata huduma bora, ya kisasa na inayokidhi matarajio. Tunataka NSSF iwe taasisi ya mfano katika uwajibikaji”, amesema Bi. Malemi.
Aidha, Bi. Malemi amewapongeza wajumbe wapya wa Bodi ya Wadhamini na kuwataka kuhakikisha Mfuko unasimamiwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa, huku akiwataka wajumbe wa Baraza hilo kuwa chachu ya mabadiliko chanya katika maeneo yao ya kazi.

Kwa upande wake, Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, amesema Mfuko unatarajia kupata mafanikio makubwa zaidi kwa kuwa umewekewa vipaumbele vinavyolenga kupanua wigo wa wanachama, kuongeza mapato, kuboresha ulipaji wa mafao na kuimarisha huduma kwa wanachama kupitia mifumo ya TEHAMA.

Awali, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Ekwabi Mujungu aliwataka wajumbe wa Baraza hilo kuzingatia kwa makini maazimio watakayoyapitisha ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Mfuko.

Bi. Flora Ndutta, akitoa neno la shukrani amesema NSSF itaendelea kutoa huduma bora kwa kutumia TEHAMA, kuwafikia wananchi waliojiajiri na kwamba wataendelea kufanya kazi kwa bidii, kwa weledi na kwa kuzingatia maadili.
Post A Comment: