Mwekezaji Wa sekta ya usafirishaji jijini Arusha Patrick Petro mulokozi amelalamikia Jeshi la Polisi Mkoa Wa Arusha kushindwa kumpa ushirikiano Wa kufungua mashitaka ili apate Mali zake ambazo ni mabasi mawili aina ya costa aliyekuwa ameyakodisha kwa kampuni ya Impala shato  inayofanya usafirisha wa abiria na mizigo kwenda nchi jirani 

‎Kijana Patrick anaeleza kuwa amesumbuka kwa zaidi ya mwaka mmoja kwenye kituo Cha polisi Cha Cental Arusha kufungua mashitaka lakin Kila alipoenda alichukuliwa maelezo na hakuna chochote kilichoendelea ikiwa nipamoja na upelelezi kufanyika na watuhumiwa wake kukamatwa

‎Hakuishia hapo Patrickanaeleza kuwa kuna baadhi ya maafisa Wa NGAZI za juu Wa Jeshi la Polisi na wasaidizi Wa ofisi ya mkuu Wa mkoa aliwaomba msaada katika kupa Mali zake  na Kila walipotaka kumsaidia walimweleeza walipigiwa kutoka ngazi za juu na kuwaeeleza waachane na swala Hilo 

‎Patrick ameeleza kuwa mtu anamlalamikia kuchukua mabasi yake bwana Edimundi Koka ni Mdogo Wake na Mbunge Wa Jimbo la Kibaha Silvester Koka ambae kaka yake huyo anatumia nafasi yake ya ubunge kuwapigia viongozi wakubwa simu na yeye kukandamizwa asipatiwe haki yake 

‎Patrick anamuomba Rais Dkt Samia na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda wamsaidie kupata haki yake 

‎Juhudi za kumpata anae lalamikiwa zimefanyika ikiwa ni pamoja na Kufika Ofisini kwake na baada ya Kufika na kuwaona waandishi Wa Habari alikataa Kuzungumza chochote na kumuagiza mtoto wake kueleza hajupo tayari Kuzungumza na waondoke 

Juhudi ya kulipata Jeshi la Polisi ziligonga mwamba huku msaidizi Wa Kamanda Wa polisi Mkoa wa Arusha aliyepokea simu alieleza kuwa  Kamanda yupo bize kwenye misafara ya viongozi iliyopo Mkoani Arusha

Share To:

Post A Comment: