Waziri wa Ujenzi Mhe Abdallah Ulega ameshukuru Maono ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuchochea na kuhamasisha uhusiano baina ya serikali na sekta binafsi yaliyosaidia kutatua changamoto ya usafiri kwa wananchi wa Kigamboni Jijini Dar E salaam.

Kwasababu ya utu, maono, uzalendo na ubunifu wa Mhe. Rais Samia, Serikali imeruhusu kampuni ya Bakhresa kutumia vivuko binafsi ili kupunguza usumbufu uliotokana na changamoto zilizovikumbuka vivuko vya serikali, wananchi wanaotoka na kwenda kigamboni walikuwa wakipata adha na usumbufu mkubwa, hivi sasa wale wanaotaka kutumia kivuko cha serikali wanatumia na wale wanaotaka kurumia vya azam nao wanatumia na kwa kiasi kiasi kikubwa, tumeondoa usumbufu wa usafiri." Mhe. Ulega ameliambia Bunge la Tanzania.

Wakati akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2025/26 Bungeni Dodoma, Waziri Ulega pia amesema Wizara yake hadi Aprili 2025, ujenzi na upanuzi wa jengo la abiria katika maegesho ya Magogoni- Kigamboni upande wa Kigamboni, awamu ya kwanza umekamilika na miradi mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Aidha Mhe. Ulega amebainisha kuwa  Wakala wa Majengo TBA unatekeleza miradi mingine ya ujenzi na ukarabati wa nyumba na majengo ya serikali ikiwemo  ukarabati wa nyumba za Viongozi wa serikali pamoja na usimamizi wa majengo 19 katika mji wa serikali- Mtumba.

Aidha sheria ya uanzishwaji wa wakala wa majengo Tanzania imehuishwa na kuruhusu wakala kuhusisha sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi yake pamoja na kuwauzia na kuwapangisha nyumba wasio watumishi wa umma kwa bei ya soko, wakala huo ukiainisha pia maeneo yake  yaliyoiva kibiashara (Prime areas) katika Mikoa ya Dar Es salaam, Arusha, Dodoma na Mwanza kwaajili ya kuyaendeleza kaa njia ya ubia pamoja na mikopo kutoka kwenye Taasisi za kifedha, Waziri Ulega akiwakaribisha wawekezaji wote wa ndani na nje ya nchi kuwekeza na wakala huo.

Share To:

Post A Comment: