Mradi wa kielelezo wa Ujenzi wa daraja la Kigongo- Busisi Mkoani Mwanza umekamilika kwa asilimia 99, ambapo kulingana na Wizara ya Ujenzi kupitia kwa Waziri wake Mhe. Abdallah Ulega ameliambia Bunge la Tanzania kuwa matarajio ni kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni rasmi katika uzinduzi wake hivi Karibuni.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Ulega leo Jumatatu Mei 05, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2025/26, akieleza kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutakuwa faraja kubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa ambao wamekuwa wakitumia muda wa takribani saa mbili kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine.
"Baada ya daraja hili kukamilila muda wa kuvuka unatarajiwa kupungua kufikia wastani wa dakika tatu. Aidha daraja hili linategemewa kuongeza shughuli za kiuchumi ndani na nje ya Mikoa ya kanda ya ziwa na nchi jirani lakini pia daraja hili litamywa mojawapo ya alama na fahari ya taifa letu kwani kwa urefu wake wa Kilomita 3.2 litakuwa daraja refu zaidi katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki na kati." Ameongeza Waziri Ulega.
Katika hatua nyingine Waziri Ulega ameeleza kuwa mara baada ya kuzinduliwa kwa daraja hilo na kuanza kutumika kikamilifu, vivuko vyote vilivyokuwa vinatumika kwenye eneo hilo la Kigongo-Busisi vitapelekwa katika maenei mengine nchini yatakayokuwa na uhitaji wa huduma hiyo.
Waziri Ulega kadhalika amemshukuru na kutoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye si tu amelup gharama zote kwa wakati kwa mkandarasi wa Ujenzi huo lakini pia amekamilisha mradi huo ambao ulikuwa ni ndoto ya Mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Post A Comment: