"Mhe. Spika katika mwaka wa Fedha 2024/25, miradi ya barabara kuu iliyopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa barabara zenye urefu wa kilometa 385 kwa kiwango cha lami, ukarabati wa kilometa 35 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa madaraja 17, ukarabati wa daraja moja (1), kufanya maandalizi ya ujenzi wa madaraja tisa na kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa madaraja mawili. Hadi kufikia Aprili, mwaka 2025, utekelezaji wa malengo hayo ni kama ifuatavyo:

Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 109.49 umekamilika na ujenzi wa kilometa 275.51 unaendelea. Ujenzi wa madaraja matano unaendelea na ujenzi wa madaraja  matano upo katika hatua za maandalizi.

Jumla ya kilometa 98.89 za barabara za mikoa zilijengwa kwa kiwango cha lami na jumla ya kilometa 192.89 zilikarabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Aidha, ujenzi/ukarabati wa madaraja madogo 12 kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na 13 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Mhe. Spika  miradi saba ya barabara iliyokuwa itekelezwe kwa utaratibu wa EPC +F sasa inatekelezwa kwa utaratibu wa ‘sanifu na jenga’  (Design and Build). Hadi sasa,  maboresho ya kimkataba (addendum) ya miradi sita yameshasainiwa. Aidha, mradi mmoja wa Igawa – Songwe – Tunduma sasa utatekelezwa kwa njia ya PPP, ambapo taratibu za kusaini mkataba zinaendelea. 

Sambamba na hilo, Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake mkoani Tanga aliagiza ujenzi wa barabara ambayo hapo awali ilikuwa itekelezwe kwa utaratibu wa  EPC+F kutoka Kiberashi hadi Singida sasa utekelezwe kwa utaratibu wa  PPP. Tayari TANROADS na TPA wameanza majadiliano ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa agizo hilo." Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2025/26 leo Mei 05,2025

Share To:

Post A Comment: