Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini bw.Joseph Modest Mkude  akizungumza na Makundi ya wanawake na Vijana ambao hawapo pichani wakati wa Semina ya Elimu ya fedha iliyofanyika katika ukumbi wa AM MALL mkoani Arusha.

Benki ya CRDB  kupitia programu maalum ya kuwezesha Vijana na Wanawake inayojulikana kama Imbeju iliyopo chini ya taasisi Tanzu ya CRDB  Foundation imetoa elimu  ya fedha kwa watu takribani Milioni Moja,hapa nchini.

Aidha katika kipindi cha mwaka 2023 hadi Januari 2025 benki ya CRDB imetoa mikopo yenye thamani ya  shilingi trilioni 10.946,kwa sekta zote hapa nchini kwa wajasiriamali wa Awali na Kati.

Akizungumza wakati semina ya vikundi vya wajasiriamali zaidi ya 130 ambavyo watu takribani 1000 wameshiriki,Mkuu wa kitengo cha biashara kutoka benki ya CRDB bw.Boma Raballa alisema kuwa benki hiyo imeshatoa mikopo yenye jumla ya shilingi trilioni 10.946 kwa sekta zote hapa nchini kwa wajasiriamali wa Awali na Kati.

Bw.Raballa alisema kuwa kupitia Taasisi Tanzu ya CRDB Foundation jumla ya mitaji wezeshi yenye thamani ya shilingi bilioni 20 imeshatolewa na wanufaika wakubwa ni Wanawake na Vijana.

"Hii mikopo ni utekelezaji wa ilani ya chama Cha mapinduzi na mtazamo sahihi wa serikali wa kuhakikisha kuwa inatafuta namna Bora ya kuisaidia jamii kukuza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia mikopo hii"Alisema Bw.Raballa

Kwa Upande wake mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini bw.Joseph Modest Mkude ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa semina hiyo ni muhimu na ni Juhudi za serikali ya Awamu ya Sita chini ya Raisi Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuboresha maisha ya wananchi kwa kutoa kipaumbele kwa Wanawake na Vijana.

Pia alisema kuwa Ushauri na Mafunzo ya namna ya kukuza biashara kutoka kwa wataalamu hao ni miongoni mwa sehemu ya uhakika za kupata elimu ya fedha na kufanikisha mipango Yao.

"Uwepo wa Taasisi ya CRDB Foundation hapa Arusha Leo ni fursa kwa Wanawake na Vijana Wetu kuelimika na kufanya biashara kwa malengo makubwa, ambayo yatafanikiwa kukuza kipato binafsi,kaya na taifa kwa ujumla naomba muendelee kushirikiana na benki hii"Alisema Mkuu wa Wilaya

Mheshimiwa Mkude aliwataka kutumia fursa hiyo kwa kuwa ni adimu na kuitumia vyema katika kuwa mahiri katika biashara na maisha kwa Ujumla,kwa kuwa elimu ya fedha ni ngao ya kukabiliana na umaskini ambao kila mmoja anauchukia.

Programu hii ya Imbeju ambayo ipo chini ya Taasisi Tanzu ya CRDB Foundation Ina lengo la kusaidia Wanawake,Vijana na Makundi Maalumu ili kuboresha maisha Yao na uchumi kwa ujumla.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo ambaye ni kiongozi katika kikundi cha wanawake akipokea fundi ya mfano iliyotolewa na benki ya CRDB ambayo ni mikopo kwa wanawake na vijana


Viongozi waandamizi wa Benki ya CRDB wakiwa na washiriki wa semina hiyo katika picha ya pamoja
Share To:

Post A Comment: