Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo Machi 7, 2025 umekabidhi vifaa vya Uzazi (Delivery Kit) kwa wamama Wajawazito katika Kituo cha Afya Nandagala wilayani Ruangwa.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo Machi 7, 2025 umekabidhi vifaa vya Uzazi (Delivery Kit) kwa wamama Wajawazito katika Kituo cha Afya Nandagala wilayani Ruangwa.Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo Machi 7, 2025 umekabidhi vifaa vya Uzazi (Delivery Kit) kwa wamama Wajawazito katika Kituo cha Afya Nandagala wilayani Ruangwa.
Vifaa hivyo vimehususisha kibegi chenye vifaa vyote vya vinavyomuwezesha mama mjamzito kujifungua salama.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Mhe. Andrew Chikongwe wakati akikabidhi vifaa hivyo, ametoa wito kwa wamama hao kuvitunza vifaa hivyo mpaka muda wa kujifungua utakavyofika na wasiviuze kwa watu wengine kwani vinatunzika na wala haviharibiki.
Nao, wanufaika wa vifaa hivyo wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwathamini na kuwajali kwani wamewatua mzigo wa kununua vifaa hivyo.
Post A Comment: