KATIBU wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla amemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu na Chama chake waombe radhi wazanzibar kwa kuwabagua kwa kile alichosema kwamba Wabunge 50 wa Zanzibar kura zao ni sawa na Jimbo moja la Tanzania Bara.
Makalla ameeleza hayo leo Machi 8, 2025 wakati akizungumza katika mkutano wa ndani uliofanyika kuzungumza na viongozi wa chama ngazi ya shina, tawi, kata na Wilaya katika Wilaya ya Kigamboni Dar es salaam, ikiwa ni mwisho wa ziara yake ya siku tano mkoani humo.
Aidha, Makalla amesema watanzania ni mfano kwani nchi yetu inamakabila mengi lakini hakuna ubaguzi, ameongez akuwa kutokana na muungano uliopo katika CCM na kiongozi yeyote anayetokana na CCM kwa nafasi zote lazima aape kulinda muungano uliopo.
Makalla amedokeza kuwa kitendo cha Lissu kusema kwa upande wa Zanzibar wakichaguliwa wabunge 50 ni sawa na kura za jimbo moja sio sawa na kuwa ni ubaguzi mkubwa.
"Lissu aliongea na wahariri alisemaZanzibar kule wakichaguliwa wabunge 50 nisawa sawa na kura za jimbo moja la Tanzania Bara, huu ni ubaguzi mkubwa, nidharau na hajaanza leo, hiki ndicho chama ambacho siku kikishika madaraka muungano utakufa,” amesema Makalla.
Ameongeza; “Vipo vyama vya siasa vinaubaguzi kwa kuwagawa watu kwa makabila, kuwagawa watu kwa utanganyika na uzanzibar na hili nimeshuhudia hivi karibuni bila woga Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu akiwadharau wazanzibar bila woga.Mimi nataka wazanzibar waamke waiangalie CHADEMA, hiki sio chama ambacho kitakuja kudumisha muungano na hapa namtaka Tundu Lissu na CHADEMA watoke hadharani wawaombe radhi wazanzibar, jambo hili haliwezi kuachwa hivi hivi”.
#CCMImara
#VitendoVinasauti
#KaziIendelee
Post A Comment: