Viongozi wa Dini wa madhehebu mbalimbali Jijini Dodoma kwa sauti moja wamempongeza Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa kazi kubwa ya kuhamasisha shughuli za maendeleo na kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya serikali inayoleta matokeo chanya kwa jamii.

Hayo yamesemwa jana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Karmel Dkt. Evance Chande wakati wa ufunguzi wa mkutano mkubwa wa Injili wa maombi kwa ajili ya Taifa Tanzania na maombi mahsusi kwa serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt .Samia S. Hassan.

“Sisi viongozi wa Dini tuna wajibu wa kuhakikisha kwamba misingi ya Taifa Tanzania inasimamiwa na kulindwa kwa nguvu kubwa kama ilivyoasisiwa na waasisi wa Taifa hili Hayati Mwl. Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Aman Karume.

Mungu ameijaalia Tanzania amani,upendo na mshinkamano.Tuzitunze hizi tunu kwa kizazi cha leo na kijacho pia.

Tuna Rais msikivu,mnyenyekevu na mpenda maendeleo.Tunaendelea kumuombea kwa Mungu wetu ili kazi nzuri anayoifanya ya kuwaletea maendeleo watanzania iendelee kwa viwango na kasi ya ajabu.

Pia kipekee leo tumeona tutoe tuzo kwa Mbunge Anthony Mavunde ambaye amekuwa mstari wa mbele kwenye shughuli nyingi za kijamii na hivyo kuwa kimbilio la wanaDodoma wengi”Alisema Askofu Mkuu Dkt. Chande

Akitoa salamu zake,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Anthony Mavunde amewashukuru viongozi hao kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Mh Rais Samia na kuwaomba kuendelea kuhubiri juu ya Amani,Upendo na Mshikamano miongoni mwa Watanzania.

AidhaWaziri Mavunde alitumia pia fursa hiyo kuwahamasisha waumini wote kutumia nafasi ya kujiandikisha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kabla zoezi kufungwa rasmi tarehe 20.10.2024








Share To:

Post A Comment: