Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert John Chalamila, ameendelea na ziara yake ya usiku kwa usiku leo, Oktoba 23, 2024, ikiwa ni siku ya pili ya ziara ya ukaguzi wa miundombinu na utoaji wa huduma nyakati za usiku katika Wilaya ya Kinondoni.
Ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo unakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya awamu ya sita, chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
RC Chalamila akiwa wilayani humo amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Bagamoyo ya mwendo kasi inayounganisha maeneo ya Tegeta, Mwenge, Ubungo, na Mbezi. unaotarajiwa kukamilika ndani ya miezi nane na hadi sasa ujenzi huo umefikia kwa asilimia 61% ya ukamilifu na itakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Bunju na maeneo jirani kwa kuboresha huduma za usafiri.
Pia Mkuu wa Mkoa ametembelea Shule ya Sekodari Mabwe Tumaini na kuzungumza na wanafunzi, akiwahimiza kusoma kwa bidii kwani Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameboresha mazingira ya kujifunzia. Aidha, amewataka kuepuka vitendo viovu shuleni. RC Chalamila pia ameahidi kuwazawadia wanafunzi mchele, ng'ombe, na soda vilevile shilingi laki 3 kwa washindi wa kwanza wa mashindano ya mpira wa kikapu.
Akiwa ziarani humu RC Chalamila amepita kukagua mwenendo wa urendaji kazi katika kituo cha polisi cha mabwe pande. ametoa maagizo ya kutomchekea mtu yeyote anayedhamilia kuharibu amani ya nchi yetu na kushughurika na wavunjifu wa amani kama wezi,vibaka, sambamba na sheria za nchi,pia kushughulikia biashara haramu zinazoingia nchini kwa magendo kama madawa ya kulevya.
Mwisho wa ziara hiyo ya usiku wa kuamkia tarehe 24 Oktoba ametembelea pia hospitali ya Wilaya ya Mabwepande iliyojengwa zaidi ya milioni 400 ghorofa tofauti tofauti zilizomo kituoni humo
“sekta ya Afya ni sekta muhimu na haiitaji siasa” asema Chalamila
hivyo, watoa huduma za afya wanapaswa kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora.
Post A Comment: