Na Okuly Julius Chamwino ,DODOMA


HALI ya Upatikanaji huduma ya maji Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma imefikia asilimia 91 huku mikakati ikiendelea kuboresha huduma hiyo.

Akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazngira (DUWASA) na viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Janeth Mayanja amewasisitiza viongozi wa mitaa kushirikiana na jamii kulinda vyanzo vya maji.

Amesema huduma ya maji ni muhimu kwa wananchi kwasababu wakikosa hawawezi kufanya kitu chochote.


“Tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu upatikanaji wa maji ni muhimu sana. Niwasisitize na viongozi wa vijiji kuhakikisha mnawaeleza kuhusu miradi inayotekelezwa na serikali na ambayo ipo katika mkakati wa kutekelezwa ili kujenga uelewa na kupunguza malalamiko,”amesema Mayanja

Ameongeza kuwa:”Rais Dk.Samia Suluhu Hassan lengo lake ni kuona wananchi wanapata huduma ya maji ndio maana amekuwa akitoa fedha kwa ajili ya kulipa fidia ili miradi itekelezwe ,”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph, amesema lengo la kikoa hicho ni kupeana taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji Chamwino na kusikiliza changamoto zinazosababisha huduma hiyo kuwa chini ya kiwango.

“Lengo la kukutana hapa ni kufahamiana na kusikiliza changamoto zinazokwamisha jitihada za kuwafikia wananchi na kuweka mikakati ya uboreshaji wa hudu,”amesema Mhandisi Aron

Naye Meneja wa DUWASA Kanda ya Chamwino George Mwakamele amesema upatikanaji wa maji umefikia asilimia 91 na mikakati yao ni kufikia 95 ifikapo mwaka 2025.

Amesisitiza kuwa katika kipindi cha miaka mitatu serikali imetoa sh.bilioni 1.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chamwino George Malima ameishauri DUWASA kuanzisha mfumo wa kulipa kabla ya kutumia ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.

DUWASA inafanya mikutano mbalimbali na viongozi wa Serikali za Mitaa katika ngazi ya kijiji mpaka Halmashauri ,wakiwemo wenyeviti na watendaji wa vijiji,kata,madiwani na wakurugenzi wa wilaya kulingana na maeneo ambayo Mamlaka hiyo inahudumia ndani ya Mkoa wa Dodoma.









Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: