Chuo Cha Uhasibu Arusha kwa kushirikiana na  kampuni ya Rethinking Tourism Africa wamefanya kongamano la maadhimisho ya siku ya utalii duniani  leo September 27,2024 kwa kushirikisha wadau wa sekta hiyo katika hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii mheshimiwa Dastan Kitandula amesema kuwa sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika pato la taifa kwa asilimia 15.

Aidha amesema kuwa sekta hiyo pia inachangia fedha za kigeni kwa silimia 25 huku akisisitiza kuwa serikali inaendelea na mipango ya kufungua maeneo ya kusini mwa nchi ili kuendelea kukuza sekta hiyo muhimu kwa mustakabali wa Uchumi wan chi.

“Tunaendelea na Jitihada mbali mbali za kufungua maeneo mengine ambapo tunaelekea upande wa kusini na kuhakikisha pia tunateka masoko mengine ya kimataifa kwa sasa tayari tunafanya vizuri katika soko la Brazil,Asia,Marekani,Europe,China na India”Alisema Kitandula

Pia tutaendelea kuboresha Miundombinu ya Barabara na viwanja vya ndege ili kuhakikisha kuwa wanaotumia huduma hizo wanatumia mazingira rafiki na kufurahia huduma hiyo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Profesa Eliaman Sedoyeka amesema kuwa chuo hicho kina vitivo vitano ambapo ina idara inayohusika na mambo ya Utalii hivyo idara hiyo kwa kushikirikiana na wadau wameandaa kongamano hilo (Arusha International Tourism Conference and Expo) ambalo lilianza rasmi mwaka 2023 na litaendelea kufanyika kila mwaka.

“Katika kongamano hili tunaleta wanazuoni na wadau mbali mbali kujadili muktadha mzima wa sekta ya utalii kuanzia masomo,utafiti,na hasa hususani katika  soko,sasa sisi kama wadau kwa kuzingati utalii na biashara  hii kinachouzwa ni Ujuzi mtu akija akiondoka aondoke na taswira nzuri ya nchi,sasa kwa kufanya hivyo rasilimali nis waka muhimu sana”alisisitiza sedoyeka.

Kutokana na hali hiyo amesema chuo hicho kinatoa mtaala wa shahada ya Utalii na uanagenzi  ambapo wanafundisha wanafunzi kwa vitendo jinsi ya kuhudumia sekta hiyo kuanzia kupokea wageni mpaka uendeshaji wa sekta ya utalii kwa ujumla.











Share To:

Post A Comment: