Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira  Vijijini (RUWASA) wilayani Karatu imewatua ndoto kichwani zaidi ya wananchi 6000 wa kijiji cha Chemchem Kata ya Rhotia Wilayani Karatu.

Kupatikana kwa maji hayo kumepunguza magonjwa yatokanayo na kutokunywa maji safi na salama,uimarishaji wa usafi wa mazingira ikiwemo shughuli za kiuchumi ambapo Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Arusha Mhandisi Joseph Makaidi amesema  maji hayo pia yamewezesha mifugo kunywa maji na kuondoka adha kwa wafugaji kutembela umbali mrefu kutafuta maji kwaajili ya mifugo haswa kipindi cha kiangazi.

Mhandisi Makaidi amesema mradi huo umeshirikisha wananchi pamoja na wahisani (Youth with a mission) uliojengwa kwa gharama ya sh,milioni 590,048,142.10 ambapo wananchi wamechangia sh,25,000,000 ,wahisani sh,8,000,000 huku serikali kuu ikitoa sh,557,048,142.10.

Amesema mradi huo lita 7,000 kwa saa,ikiwa na vituko vya uchoteai maji 18  kwa sasa mradi huo umekamilika kwaasilimia 100 na kwa sasa tayari chombo cha watoa huduma za ngazi ya jamii kimeundwa kwaajili ya usimamizi endelevu wa maji hay

Wakati huo huo, Kiongozi wa wakimbiza mwenge Kitaifa, Godfrey Mnzava akizundua mradi huo  amepongeza juhudi zinazofaywa na Ruwasa katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama na kuwaagiza kulinda miundombinu hiyo ili isiharibike.

"Serikali unasogeza huduma za miundombinu kwa wananchi hivyo muitunze sambamba na chombo chenu ya usimamizi wa majingazi ya jamii(CBWSO) mkilinde.












Share To:

Post A Comment: