Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho KikweteRais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameipongeza Tume ya Ushindani (FCC) kwa utekelezaji wa Sheria ya Ushindani inayolenga kuzuia athari za ukiritimba katika soko pamoja na kuondoa vizuizi vya uwekezaji kwa wawekezaji.

 

Dkt. Kikwete ametoa  pongezi hizo leo alipotembelea banda la FCC lilipo ndani ya Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ambapo  huduma za elimu na majukumu ya FCC zinatolewa kwa wadau na wananchi wanaotembelea banda hilo.

 

"Watanzania wakipata elimu hii ya bidhaa bandia itasaidia sana kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la bidhaa bandia ikiwa ni pamoja na kusaidia kukua kwa biashara na ushindani katika soko na wananchi watapata bidhaa halisi na salama” amesema Dkt. Kikwete.

 

Aidha, Dkt. Kikwete amewapongeza wafanyakazi wa FCC kwa kazi nzuri wanazofanya hususan utoaji wa elimu ambap hizo zitawasaidia wananchi hao kupata uelewa wa kina katika kutambua bidhaa bandia.

 

Maonesho ya 48 yBiashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwl. Julius K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, Kurasini Jijini Dar es Salaam yalifunguliwa rasmi na Mhe. Mhandisi. Filipe Jacinto Nyusi, Rais wa Msumbiji akiwa na mwenyeji wake Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani tarehe 3 Julai, 2024. 






Share To:

Post A Comment: