Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tanga Kimeonesha kutoridhishwa na kitendo cha Gari ya Halmashauri ya wilaya ya kilindi kumgonga Mtoto na kumtelekeza bila ya Msaada ambapo chama hicho kimeagiza Halmashauri hiyo kuhakikisha inatoa Msaada wa huduma stahiki pamoja na gharama zote walizotumia wazazi wa mtoto huyo

Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoani Tanga ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika katika kijiji cha kisangasa kata ya Kisangasa wilayani Kilindi Mkoani Tanga

Changamoto hiyo imeibuliwa na Baba mzazi wa mtoto huyo ambaye amesema Mwaka 2023 mtoto wake aligongwa na gari ya Halmashauri ya Kilindi, ambapo tangu mtoto huyo agongwe hakuna msaada ambao ameweza kupatiwa na Halmashauri hiyo.

Anasema mtoto huyo alifikishwa katika Hospitali ya Rufaa Bombo mkoa wa Tanga, alijitahidi kutafuta baadhi ya Viongozi akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Omary Kigua bila mafanikio yoyote ambapo bado anaendelea na jitihada za kutafuta msaada ili mtoto huyo aweze kutibiwa.

Katika Mkutano huo wa Hadhara Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Tanga aliweza kuchangia Jumla ya Kiasi cha Laki mbili kwa ajili ya Matibabu huku mbunge wa Jimbo akichangia Elfu Hamsini pekee




Share To:

Post A Comment: