Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imetembelea na kukagua miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) jijini Dar es Salaam.


Miradi iliyotembelewa na Kamati hiyo ni mradi wa Morocco Square pamoja na miradi ya Samia Housing Scheme na ule wa 711 iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ameongoza ujumbe wa Wizara ya Ardhi pamoja na ule Shirika la Nyumba la Taifa katika ziara hiyo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge iliyoongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Timotheo Mzava.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geophrey Pinda ameishukuru kamati ya Bunge kwa ushauri inayoutoa kwa wizara alioueleza kuwa, umeisaidia wizara na taasisi zake kuboresha shughuli zake.

Amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuwezesha miradi ya Shirika la Nyunba la Taifa iliyosimama kwa muda mrefu kuendelea.

Share To:

Post A Comment: