Jumla ya watu 29,000 wamechunguzwa magonjwa mbalimbali katika kambi maalumu ya madaktari bingwa inayofanyika katika viwanja vya Sheik Amri Abed vilivyopo mkoani Arusha.

Wagonjwa waliochunguzwa kwa upande wa magonjwa ya moyo ni 1,534 watu wazima wakiwa 1,379 na watoto 155 wagonjwa 187 wanapelekwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kupatiwa matibabu ya kibingwa ambapo  gharama zote za matibabu hayo  zinalipwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizugumza kuhusu kambi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt. Peter Kisenge alisema zoezi la upimaji na matibabu limeenda vizuri ambapo wananchi wamepata fursa  ya kuhudumiwa magonjwa mbalimbali na madaktari bingwa waliobobea  katika magonjwa ya binadamu.

Dkt. Kisenge wagonjwa 187 wamekutwa na matatizo mbalimbali ya moyo katika hao watoto 53 wanatakiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo hii ni kutokana  na valve zao pamoja na mishipa ya damu ya moyo kupata matatizo .

“Watoto hao wote matibabu yao yatagharamiwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja inagharimu kiasi cha shs.12 milioni na hivyo wananchi mnapaswa kuona ni jambo la kishujaa sana lililofanywa na Rais wetu kwani kwa kawaida mwananchi wa kawaida ni ngumu sana kumudu hizo gharama hizo”, alisema Dkt. Kisenge.

Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktarin bingwa wa moyo alisema muda wa matibabu  hayo  umeongzwa  hadi siku ya kesho kwaajili ya kumaliza wagonjwa ambao wanaendelea kupata huduma katika kambi hiyo ili waweze kupata huduma wanayostahili.

“Takwimu zinaonyesha duniani kote kuwa asilimia kubwa ya watu wanaopoteza maisha wanatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo ya moyo hivyo elimu zaidi inahitajika kutolewa kwaajili ya wananchi kufuata mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi mara  kwa mara, kutovuta sigara, kunywa pombe kwa kiasi sambamba na kupunguza vyakula vya wanga na kuzingatia lishe bora”, alisema Dkt. Kisenge.




Share To:

Post A Comment: