NAIBU Waziri wa Afya,Dkt Godwin Mollel amemwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha {RMO}, Dkt Charles Mkombachepa na Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Longido {DMO} ,Dkt Mathew Majan kuhakikisha wanapeleka bajeti Serikali Kuu ya ujenzi wa nyumba nane za watumishi wa afya katika halmashauri ya Longido.

Mollel alitoa maagizo hayo katika Kijiji cha Wosiwosi kilichopo kata ya Gelai Lumbwa wilayani humo wakati akitembelea ujenzi wa zahanati iliyofikia asilimia 89 kukamilika na imegharimu shilingi milioni 113 hadi sasa ambapo mchango wa wananchi ni shilingi milioni 8.9,mchango wa halmashauri shilingi milioni 30 na fedha toka serikali kuu ni shilingi milioni 70.

Alisema Rais Samia Suluhu Hassan amepelekea fedha Longido kwa ajili ya ujenzi wa zahanati nane katika maeneo mbalimbali wilayani Longido na zahanati hizo ziko katika hatua ya mwisho kukamilika lakini hakuna hata nyumba moja iliyojengwa kwa ajili ya watumishi sasa shughuli haziwezi kufanyika bila watumishi wa afya.

Waziri Mollel baada ya kujionea hali hiyo alimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha na Mganga Mfawidhi wa Wilaya ya Longido kuhakikisha wanapelekaa bajeti ya ujenzi wa nyumba za watumishi katika zahanati hizo ili ziendee sambamba za ujenzi wa zahanati ili wananchi waweze kusogezewa huduma za afya karibu tofauti na ilivyo sasa.

Alisema umbali wa kutoka kijiji cha Wosiwosi hadi huduma ya Afya iliyopo Getumbeine ni umbali wa zaidi ya km 91 lakini Rais ameamuwa kutoa fedha na kusogeza huduma hiyo Kijiji lakini sisi watumishi hatuendi na wakati kwani huwezi kujenga zahanati bila kuwa na nyumba ya watumishi wa afya hilo halikubaliki na alitaka bajeti hiyo kwenda serikalini hususani Wizara ya Afya ili iweze kufanyiwa kazi na ujenzi uanze mara moja kwa maslahi ya wananchi.

‘’RMO Mkombachepa na DMO Majan fanyeni kila linalowezekana kuhakikisha bajeti ya nyumba za watumishi wa afya inakwenda serikali kuu haraka hii zahanati ikiisha nyumba nazo zimeshaanza kujengwana ujenzi wa nyumba hizo usichukue muda mrefu’’

 ‘’Huwezi kujenga zahanati bila kujenga nyumba za watumishi hali ya huku kama unavyoiona ni mbali sana kutoka Longido Mjini hadi hapa ni km 149 na wananchi ili wafuate huduma lazima wasafiri km 91 jamani tuwahurumie Rais ametimiza yake sasa sisi tunashindwaje kukamamilisha ujenzi wa nyumba wakati fedha ziko’’alisema Mollel

Naye Naibu Waziri wa Madini na Mbunge wa Jimbo la Longido Dkt Steven Kiruswa alimshukuru Rais kwa kupeleka fedha za Afya katika Jimbo hilo na zimefanya kazi iliyokusudiwa na hawakuweza kumwangusha.

Alisema hali ya mradi hadi sasa imefika asilimia 89 ya utekelezaji na kazi iliyobaki ni kutisha milango,madirisha na kuweka ceiling board ili zahanati hiyo iweze kuanza kazi lakini changamoto ni nyumba za watumishi.

Naye Mtendaji wa kata ya Gelai Lumbwa,Marko Kaleku akisoma taarifa alisema kuwa Kijiji cha Wosiwosi kina jumla ya wakazi 1,900 Kijiji hakikuwa na zahanatihivyo uongozi wa wilaya baada ya kuona changamotoza vifo vya mama na motto vinavyotokana na kukosekana kwa huduma ya afya katika Kijiji hicho waliamua kujenga zahanati.

Share To:

Post A Comment: