Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Godfrey Mnzava amempongeza mwenyekiti wa Uvccm mkoa wa Njombe Samuel Mgaya kwa kuwaunganisha vijana katika ukimbizaji mwenge ndani ya mkoa hadi unakabidhiwa salama mkoani Iringa.

Mnzava amesema hakuna mkoa uliowaunganisha vijana wa hamasa kama mkoa wa Njombe katika ukimbizaji mwenge jambo ambalo Mwenyekiti wa Uvccm mkoa amekuwa mfano mzuri  wa kuigwa katika mikoa mingine kwani hamasa ilikuwa kubwa.

Kauli hiyo ameitoa leo asubuhi katika kijiji cha Nyigo wilayani Mufindi wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru toka mkoa wa Njombe kwenda Iringa.
Share To:

Post A Comment: