Na.Nickson Mahundi,Ludewa.

Akipokea misaada mbalimbali kutoka katika kampuni yakuambiana Investiment mkuu wa wilaya ya Ludewa Mh.Victoria Mwanziva alisema ni wakati wa wanaludewa wanaoishi nje ya wilaya ya Ludewa kuikumbuka wilaya yao kwakuchangia shughuri mbalimbali  zakimaendeleo wilayani hao.

DC Mwanziva aliyasema haya jana wakati akipokea vifaa mbalimbali kutoka kwa Bw.Iman Haule ambaye ni Mkurungezi wa kampuni ya kuambiana Investiment ambapo iliambatana na ufunguzi wa mashindano ya Kuambiana kwa mwaka 2024 katika Tarafa ya Masasi.

Vifaa tiba hivyo vilivyotolewa katika vituo vya Afya viwili ambavyo ni kituo cha Afya Luilo na kile cha Manda ikiwa ni muendelezo wa kaulimbiu ya kuambiana investiment inayosema Rudisha furaha nyumbani.

DC Mwanziva alisema kuwa wilaya ya Ludewa ni moja ya wilaya nchini zilizojaliwa kuwa na wasomi wengi wenye nafasi mbalimbali na wafanyabiasha wakubwa nchini lakini ni wachache sana wanaoikumbuka wilaya yao katika maendeleo hivyo wakati umefika sasa kuiga mfano wakuambiana Investiment kurudisha Furaha nyumbani.

"nawaomba sana wanaludewa mliofanikiwa kimaisha kuikumbuka wilaya yenu maana Ludewa itajengwa na wanaludewa wenyewe kwani mbunge wenu anafanya kazi vizuri hivyo Serikali pekee haiwezi kamirisha kila kitu bila wadai kuweka mkono kama akina Kuambiana na wengine kusaidia Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ,hivyo nawasihi turudi nyumbani jamani na tuwekeze"alisema DC Mwanziva.

Aidha DC Mwanziva,alilimwagia sifa nyingi Group la Wilaya ya Ludewa whatsup kwakufanya makubwa ndani ya wilaya ya Ludewa ktk kuchangia vitu mbalimbali kwani group hilo limekuwa na utamaduni wa kila mwaka kufanya jambo fulani ndani ya wilaya ya Ludewa.

Akitaja mambo mbalimbali yanayoendelea kufanywa na Serikali ndani ya wilaya DC Mwanziva alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suruhu Hassan kwakuendelea kutoa fedha za maendeleo ktk miradi mbalimbali wilayani hapa alisema mpaka sasa ni miradi mingi inaendelea kutekelezwa na wananchi wanaona na wananufaika na miradi hiyo.

Akikabidhi vifaa tiba hivyo mkurugenzi wakuambiana Investiment Bw.Iman Haule alisema kuwa,imekuwa desturi yake kila mwaka kurudisha furaha nyumbani hasa katika mashindano ya mpira wamiguu yanayojumuisha timu zote za tarafa ya Masasi na kutengeneza mzunguko wa fedha kuongezeka pale yanapofanyika mashindano kwa wananchi hupata fulsa ya kufanya biashara ndogondogo na kujiongezea kipato.

Bw.Iman Haule alisema kwa mwaka huu wa 2024 ameongeza zaidi kurudisha furaha nyumbani kwakuvikumbuka vituo vya Afya kwani ameweza kushirikiana na wadau mbalimbali wamaendeleo akiwemo mwanaludewa mwenzake Bw.Merkio Ndofi pamoja na Bank ya CRDB katika kufanikisha ununuzi wa vifaa tiba hivyo pamoja na uendeshaji wa mashindano hayo ambayo huchezwa kwa muda wa miezi mitatu hadi minne.

Alisema kuwa anaungana na Mh.Mwanziva kuwakumbusha wanaludewa wengine kuikumbuka Ludewa pia kujijengea tabia ya kurudi  nyumbani mwisho wa mwaka ili kuwafanya vijana kujifunza mazuri na kuwa na bidii ya masomo kutoka kwa waliofanikiwa kwani wilaya ya Ludewa imejaliwa kuwa na watu wanaojiweza katika nyanja mbalimbali .

Share To:

Post A Comment: