Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amepokea msaada wa vifaa tiba mbalimbali vilivyotolewa na kampuni ya Kuambiana Investment ambavyo vimelenga kuhudumka kituo cha afya Kata ya Luilo na Manda ambapo miongoni mwa vifaa hivyo ni magodoro, vitanda, baiskeli za wagonjwa pamoja na mashuka.

Akipokea msaada huo Mwanziva amempongea mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Imani Haule almaarufu kama Kuambiana huku akiwaasa wazawa wa Wilaya hiyo wanaoishi nje na ndani ya Wilaya kuunga mkono juhudi za maenedeleo zinazofanywa na serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujitoa katika kuchangia maenedeleo mbalimbali na kufanya mabadiliko yenye tija.

Aidha kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni hiyo Imani Haule amesema kampuni yake imetimiza miaka 17 tangu kuanzishwa kwake na miaka 5 tangu aanzishe ligi ya Kuambiana katika Tarafa ya Masasi Wilayani humo hivyo katika kuadhimisha miaka hiyo amaeona ni vyema kutoa mchango wake katika uboreshaji wa huduma ya afya.

" Nimekua nikitoka misaada katika sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu, na ninapendelea hasa kutoa mchango huu katika maeneo ya vijiji na si Mijini kwakuwa Mijini Kuna wadau wengi wa kuchangia maendeo kuliko vijijini hivyo nawaasa wanaludewa wenzangu tuungane kwa pamoja katika kuiletea maenedeleo Ludewa yetu kwakuwa maenedeleo Bora yanahitaji kujengwa na sisi wenyewe". Amesema Kuambiana.

Sanjari na hilo pia kampuni hiyo ilizindua ligi kwa msimu huu huku mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva ambaye aliambatana na mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Sunday Deogratius , mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Stanley Kolimba, katibu mwenezi Shukrani Kawogo pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali.

Share To:

Post A Comment: