Katika Maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani  yanayoadhimishwa Mei 20 ya kila mwaka, Wakala wa Vipimo Mkoa wa Geita imeendelea kuwafikia wadau mbalimbali na kutoa elimu na kuwakumbusha masuala mbalimbali yanayohusu vipimo ikiwemo kuzingatia sheria ya vipimo.

Akizungumza na wajasiliamali katika maeneo tofautitofauti ya viwanda vya  kuzalisha mchele Mjini Geita,  Afisa  Vipimo  Mkoa wa Geita Mohammed Masoud amesema Taasisi ya Vipimo  kupitia maadhimisho imekuwa ikikutana na wadau kwa lengo la kutoa elimu pamoja na kukumbushana mambo mbalimbali.


“Tumekutana na wadau wetu na tumewasisitiza watumie vipimo sahihi ambavyo vimekaguliwa na wakala wa vipimo na kuhakikisha wanaweka stika lengo letu ni watu kupata kitu kilicho sahihi sisi tunaamini wakitumia vipimo sahihi vitawasaidia kuinuka kiuchumi na kukuza vipato vyao na vya Familia” Mohammed Masoud Afisa vipimo Mkoa wa Geita.



Aidha Masoud ametoa ongeza msukuma zaidi kwa wafanyabiashara kuhakikisha wao wanakuwa mstari wa mbele kwa kudhibiti tabia ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma jitihada za wakala wa vipimo na kwamba wanatakiwa kuwa waaminifu na kutumia elimu waliopatiwa kuwa mabalozi kwa watu ambao wamekuwa wakichezea Mizani.



Baadhi ya wajasiliamli kwa nyakato tofauti wamewapongeza Wakala wa vipimo kwa kuwafikia na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vipimo.

“Kiukweli tunawashuru sana Wakala wa vipimo kwa elimu ambayo wameitoa kwani tumejua ni namna gani ya kuhakikisha mizani yetu inakuwa vizuri kwa nia ya kuepusha tabia ya kumpunja mteja”Sauda Salum Mfanyabiashara.

Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Tunapima leo kwa kesho endelevu, ukimbebesha zaidi ya kilo 100 sio kwa maendeleo endelevu na afya pia’’

Share To:

JOEL MADUKA

Post A Comment: