Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amefanya kikao na Uongozi wa Wilaya ya Ludewa wakiongozwa na Mhe. Victoria Mwanziva pamoja na Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme ya Madope iliyopo Wilayani Ludewa ambapo hapo wamejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Makubaliano kati ya Shirika la Umeme Nchini TANESCO ndani ya Mkoa wa Njombe kuwa tayari kushirikiana na Kampuni ya Uzalishaji wa Umeme Madope Kutoa huduma kwa Wananchi wanaotumia  Umeme unaozalishwa na Kampuni hiyo.

Aidha, Mhe. Anthony Mtaka amesema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020/2025 Kuhakikisha Mkoa wa Njombe ifikapo Mwaka 2025 utekelezaji wa Ufikishaji Umeme kwenye Vijiji vyote vya Mkoa wa Njombe uwe umekamilika kwa Asilimia mia moja.

Share To:

Post A Comment: