Ashrack Miraji Same Kilimanjaro

Katibu Tawala wa wilaya ya Same, Upendo Wella, ameyasema hayo wakati akimwahakilisha Mkuu wa Wilaya ya Same Kaslida Mgeni kwenye kuhitimisha Umoja wa Michezo na Taaluma shule za Sekondari Tanzania (UMISETA). Nidhamu ni jambo la msingi sana katika michezo, hivyo niwaombe wanafunzi ambao mnakwenda kushiriki mashindano hayo kwenye ngazi ya Mkoa kuwa na nidhamu, hasa kwa kila kile unachofundishwa na kumuheshimu kila mtu ambaye utakutana naye kwenye michezo.

Sambamba na hilo, niwaombe pia wanafunzi ambao mnashiriki Mashindano ya UMISETA, kuendelea kujikita zaidi kwenye masomo yenu ili kutimiza ndoto zenu kwenye maslahi mapana ya Taifa letu. Michezo inaambatana na elimu; unakuta sasa hivi baadhi ya vijana wengi ambao wanashiriki kwenye michezo mbalimbali wamepata mafanikio makubwa. Amesema Upendo Wella, Katibu Tawala.

Pia, ameendelea kuwasisitizia walimu, wafanyakazi, na wanafunzi kudumisha na kuendeleza michezo, maana michezo ni afya, pia ajira, na hudumisha mahusiano mazuri kwa vijana wetu. Hivyo, michezo inaleta maendeleo makubwa katika Taifa letu. Ndiyo maana tunamuona Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anavyotoa hamasa kubwa kwa timu zetu hapa nchini kwenye mashindano tofauti ndani na nje ya nchi.


Share To:

ASHRACK

Post A Comment: