mwenyekiti wa RUNALI Odas Mpunga akiongea na waandishi wa habari wakati wa utoaji tuzo za waliofanya vizuri kwenye elimu msingi na sekondari pamoja tuzo za wadau waliochangia maendeleo kwenye sekta ya elimu mkoa wa Lindi.


Na Fredy Mgunda, Lindi.


CHAMA kikuu cha ushirika mkoa wa Lindi (RUNALI) kinachohudumia wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale kimetumia zaidi ya millioni 38 kuboresha sekta ya elimu katika wilaya hizo.

Akizungumza na mwandishi wa habari, mwenyekiti wa RUNALI Odas Mpunga alisema kuwa katika msimu wa mavuno wa mwaka 2023/2024 wametoa zaidi ya shilingi millioni 38 kwa ajili kuboresha miundo mbinu ya elimu msingi na sekondari katika wilaya tatu za mkoa wa Lindi.

Mpunga alisema kuwa kila mwaka chama cha ushirika RUNALI kimekuwa kinarudisha kwa jamii sehemu ya faida wanayoipata baada ya mauzo ya mazao kwa msimu husika.

Alisema kuwa wakulima wanaotumia kuuza mazao kupitia chama cha RUNALI wamekuwa wanapata faida kulinga na thamani ya mazao yao ambayo yanakuwa yameongezewa thamani na chama hicho.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: