Askofu Mkuu wa Kanisa la Calvary Assemblies of God, Mtume Dkt. Dunstan Maboya akiambatana na Viongozi wengine wa kanisa hilo wameongoza maombi Maalum ya kumuombea Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda na kuwatakia mafanikio mema kwenye kuwatumikia wananchi.

Askofu Dkt. Dunstan Maboya amefika Ofisini kwa Mhe. Paul Makonda, mkuu wa Mkoa wa Arusha akiambatana na Mchungaji Daniel Safari na Nabii Joshua Alamu ambaye ni Rais wa Baraza la Mitume na Manabii nchini Tanzania.

Viongozi hao wa dini Wakiongozwa na Askofu Maboya wameiombea pia mihimili yote ya nchi kwa maana ya Bunge, Mahakama na Serikali na kuwataka kutenda Haki katika kuwatumikia Watanzania.

Aidha Baba Askofu Dunstan Maboya ametumia fursa hiyo kumualika Mhe. Mkuu wa Mkoa kwenye Tamasha kubwa la Muziki wa Injili linalotarajiwa kufanyika Juni 2 mwaka huu Jijini Arusha likitanguliwa na Kongamano la dini linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei mwaka Huu.
Share To:

Post A Comment: