Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul C. Makonda ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya ya Karatu iliyojengwa katika kijiji cha Changarawe Kata ya Daa Tarafa ya Karatu ambayo imeshaanza kutoa huduma tangu Januari 23 mwaka huu wa 2024.

Akizungumza na DMO Dkt. Victor Kamazima pamoja na viongozi wengine hospitalini hapo, RC Makonda amehimiza kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri na Taasisi mbalimbali za kidini ambazo zimetoa mchango mkubwa katika sekta mbalimbali nchini hasa sekta ya Afya.

" _Tuna taasisi za dini zimetoa mchango mkubwa sana kwenye sekta mbalimbali hasa katika sekta ya Afya sasa kujenga kwetu hospitali tusiwe na kiburi cha kuwadharau, tengenezeni mahusiano mazuri kiasi kwamba hata mkiwa na changamoto mkaweza kusaidiwa au nyie kuwasaidia...lengo la Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuwasaidia watanzania katika kila sekta hasa Afya kwakuwa ndio inabeba uhai wa mwanadamu_ ..." Alisema RC Makonda

Akisikiliza changamoto mbalimbali za wanachi wanaopatiwa huduma katika hospitali hiyo amepokea kilio cha upungufu wa dawa ambapo alimtaka Dkt. Amani (incharge wa hospitali) kutolea majibu ambapo alisema changamoto hiyo ipo japo si kwa ukubwa lakini wamekuwa wakiendelea kuhakikisha changamoto hiyo inakwisha.

Sambamba na hilo, RC Makonda alipokea changamoto ya kutokuwepo kwa umeme wa ziada iliyotolewa na mmoja kati ya mwananchi ambapo kwa majibu ya Dkt. Amani alisema tayari wameshanunua jenereta la ziada kwaajili ya kuepukana na changamoto ya umeme pale ambapo ikitokea umekatika.

Akitolea majibu kuhusu malalamiko ya ufinyu wa muda wa kuwaona wagonjwa, RC Makonda ameutaka uongozi wa hospitali hiyo kutumia busara katika kukabiliana na changamoto hiyo ilikusudi wananchi wanaokuja kuona wagonjwa wao na wao wapate faraja.

"Kila pahala kuna utaratib wake lakiniwakati mwingine tumieni busara ya kutazama mazingira yenu yapoje kwa maana ya upatikanaji wausafiri na umbali na watu wengine hawana uwezi wa kulipia hoteli za karibu na hapa kwakuwa kama mnavyojua Arusha ni Mji wa kitalii gharama zake za hoteli kiasi zinakuwa juu..hivyo wakati mwingine chukueni takwimu muone muda upi watu wanakuwa wameika ili mpange mda vizuri ilikusudi wananchi kupata muda rafiki wa kutembelea na kuwaona wagonjwa wao kwakuwa ni sehemu ya faraja kwao wote_ " Alisema RC Makonda






Share To:

Post A Comment: