Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack leo, Mei 24, 2024 amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja katika eneo la Uwanja wa Ndege, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack leo, Mei 24, 2024 amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja katika eneo la Uwanja wa Ndege, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Na Fredy Mgunda, Lindi.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack leo, Mei 24, 2024 amepokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja katika eneo la Uwanja wa Ndege, Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Akitoa taarifa ya Mkoa wakati wa Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru, Mhe Telack amesema kuwa katika Mkoa wa Lindi Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa kwa umbali wa jumla za KM 1128.7 katika Wilaya 5 za Mkoa wa Lindi zenye jumla ya Halmshauri 6 huku ukitarajiwa kutembelea Miradi ya Maendeleo 53 yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 45.998 ambapo jumla ya miradi 15 itawekewa Mawe ya Msingi, miradi 13 itazinduliwa na miradi 25 itatembelewa.

Aidha, kwa kuzingatia Kauli mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 unaolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu "Uhifadhi wa mazingira na Uchaguzi wa serikali za Mitaa", Mhe. Telack ameeleza kuwa Mkoa umeweza kuongeza kasi ya upandaji miti ambapo hadi kufikia April jumla ya miti 6, 544, 230 imepandwa.

Pia, Mkoa umeendelea kushirikiana na OR- TAMISEMI katika kuhakikisha ufanyikaji wa maandalizi ya awali ikiwemo uhakiki wa vituo vya uchaguzi pamoja na kutoa hamasa na elimu kwa wananchi kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa katika mikutano mbalimbali.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: