Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amemteua Bi Christine Mwakatobe kuwa mjumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha AWSA kuanzia tarehe 13 Mei 2024. Bi Mwakatobe kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano Arusha AICC.
Sehemu ya barua ya uteuzi inaaisha kuwa Waziri Aweso amemteua Bi Mwakatobe kwenye Bodi hiyo nafasi ya mwakilishi wa watumiaji wakubwa wa maji jijini Arusha.
“ Ni matarajio yangu kuwa utaupokea uteuzi na kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha iendelee kutoa huduma bora na zenye viwango vya hali ya juu,” Waziri Aweso alinukuliwa katika barua hiyo na kusisitiza kuwa Bi Mwakatobe atatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia miogozo na maelekezo ya Wizara ,Msajili wa Hazina na Serikali kwa ujumla.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa AICC mwezi Machi mwaka huu Bi Mwakatobe ambaye kitaaluma ni mchumi na mtaalamu wa masoko, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uendelezaji na Uendeshaji wa Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro
Post A Comment: