Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) Jijini Dodoma imepokea gari nyingine ya kubebea wagonjwa hivyo kufikisha magari hayo matatu ikiwa ni sehemu ya kuboresha huduma za Afya Jijini Dodoma.

Gari hilo limekabidhiwa jana kwa uongozi wa Hospitali na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ikiwa ni utimizaji wa ahadi aliyoitoa Tarehe 22.03.2024 katika hospitali hiyo baada ya kupokea ombi la kuongezewa gari ya ziada ya kusafirishia wagonjwa.

"Nimshukuru Mhe. Dkt . Rais Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya kuboresha huduma za afya.

Nawapongeza sana Hospitali kwa huduma nzuri inayoongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Alphonce Chandika Hospitali hii inahudumia si wananchi wa Dodoma bali watanzania wote na tunapokea sifa nyingi kuhusu huduma zenu," Alisema Mavunde

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali, Dkt Alphonce Chandika amesema gari hii mpya ya wagonjwa inaweza kuhimili mazingira tofauti tofauti na hivyo kupanua wigo wa kuhudumia wananchi kwa uharaka zaidi.

Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma (RAS), Ndg. Kaspar Muya amesema gari hili la wagonjwa ni mkombozi wa vifo vya mama na mtoto kwa kuwa litasaidia kuharakisha upatikanaji wa  huduma za Afya kwa wananchi.



Share To:

Post A Comment: