Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Michael Battle (aliyekaa katikati), katika picha ya pamoja na Dkt. Felix Wandwe, ndc Kaimu Mkurugenzi (CFR), (wa pili kulia) baadhi ya Wajumbe wa Menejimenti na Wawakilishi wa Wanafunzi wakati wa ziara ya Mhe. Balozi kutembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim, 23 Mei 2024
Balozi wa Marekani nchini Tanzania, mheshimiwa Michael Battle (aliyesimama) akitoa muhadhara wa kidiplomasia kwa baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Michael Battle ( kushoto) akiwa katika mazungumzo na Dkt. Felix Wandwe, ndc Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim wakati wa ziara ya Mhe. Balozi Battle kutembea Kituo hicho.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Michael Battle (wa nne kulia) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim.

Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam 

Balozi wa Marekani nchini Tanzania, mheshimiwa Michael Battle, leo Alhamis tarehe 23 Mei 2024 ametembelea Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim (CFR).

Akiwa katika Kituo hicho, Mheshimiwa Balozi Battle amekutana na kuzungumza na Dkt. Felix Wandwe, ndc Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Dkt. Salim Ahmed Salim, kutoa muhadhara wa kidiplomasia kwa baadhi ya wahadhiri na wanafunzi wa Kituo pamoja na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali aliyoulizwa na wanafunzi.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: