1000066941


Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ameitambulisha rasmi programu ya uchimbaji visima 900 kwenye majimbo 180 ya vijijini katika kijiji cha Maescron Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara aliposhughudia kisima cha kwanza kikichimbwa.

Wizara ya Maji kupitia RUWASA inatekeleza programu maalumu ya uchimbaji visima 900 ambavyo vitachimbwa katika majimbo 180 ya vijijini kwa visima vitano kwa kila jimbo kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma ya maji.

1000066944

Programu hiyo ambayo imelenga kupunguza kero ya uhaba wa maji kwenye maeneo ambayo hayajifikiwa na huduma.

Utaratibu wa uchimbaji wa visima hivyo ni maelekezo ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika jitihada zake za kumtua mama ndoo kichwani.

Utekelezaji wa mpango huu unategemea fedha kutoka Benki ya Dunia kupitia programu ya P for R, Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) pamoja na Wadau mbalimbali.

Aidha, Programu hii kwa ujumla wake inatarajiwa kutumia zaidi ya ya shilingi Billioni 54.
1000066968
1000066953
1000066950
1000066971
1000066965
1000066962
1000066947
1000066959
Share To:

Post A Comment: