Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amekabidhi msaada wa nondo zaidi ya hamsini kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mbalizi Road Jijini Mbeya.

Nondo hizo zimekabidhiwa na Lucia Mwanasinjale Katibu wa Mbunge ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalumu Jiji la Mbeya kwa niaba ya Mbunge.

Naye Mratibu wa ofisi ya Mbunge Fatuma Bora amesema huu ni utekelezaji wa ombi la Kata ya Mbalizi Road lililoombwa kwa Mbunge na Viongozi wa Kata.

Sophia Malingumu Mjumbe kamati ya siasa Kata ya Mbalizi Road amemshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa mchango mkubwa kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa ofisi ya Chama.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mbalizi Road Mheshimiwa Adam Simbaya amesema Mheshimiwa Mahundi aliombwa kuchangia nondo thelathini lakini yeye ametoa nondo hamsini ikiwa ni zaidi ya kiwango kilichoombwa.

"Hii itakuwa ofisi ya mfano nchini kutokana na ubora wa ujenzi unaoendelea ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge la kuzitaka Kata zote Mkoa wa Mbeya kuwa na ofisi za kisasa"alisema Simbaya.

Mhandisi Maryprisca Mahundi amekuwa akichangia shughuli mbalimbali za ujenzi wa ofisi za Chama Cha  Mapinduzi kama UWT,Vijana na Jumuia ya Wazazi sanjari na kuwawezesha Wanawake kiuchumi kwa kuwagawia mitaji bure pamoja na majiko ya gesi na mitungi yake.

Mahundi amekuwa akiishi na kauli mbiu ya Taasisi ya ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF)"Twende Tukue Pamoja"

Share To:

Post A Comment: