Na Ashrack Miraji 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili Mkoani Arusha ambapo anatarajiwa kuwe Mgeni Rasmi, katika Misa maalum ya Kumbukumbu ya miaka 40 ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Edward Moringe Sokoine.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amepokelewa na Viongozi mbalimbali, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda.



 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: