Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewasihi wananchi wa Rufiji kutokupotoshwa  kuhusu mafuriko yaliyojitokeza maeneo ya Rufiji na Kibiti

"Ndugu zangu kwanza poleni sana kwa kadhia hii iliyowapata, Jumuiya ya Umoja wa Vijana tumeguswa sana na Changamoto hii ndio maana tupo hapa Viongozi wote wakuu wa Jumuiya kuendeleza maelekezo ya Mwenyekiti wetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kuja kuwafariji Ndugu zetu"

"Wana Rufiji msipotoshwe kuhusu Mafuriko haya yanayotokea, kuna wanasiasa ambao kazi yao ni kudandia Ajenda hili nalo wanalichukua kisiasa "

"Kwa sisi Vijana wadogo tunaweza tusiwe na historia nzuri ya mafuriko haya lakini wazee wetu ni mashahidi kuwa maeneo haya mafuriko yamekua yakijitokeza mara kwa mara kuanzia mwaka 1968, 1972, 1978, 2020, na sasa 2024 hivyo hawa wanaosingizia Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere wasiwalaghai hata kidogo na wawaambieni hamtaki maneno matupu"

Mwisho Ndugu Kawaida amewasihi wananchi wa Rufiji itakapotokea Wataalam wameona umuhimu wa kuhama maeneo hayo  wasisite kukubali kwani ni kwa  Usalama wao.

"Niwaombe sana Ndugu zangu wa Rufiji itakapotokea wataalam wakasema tuhame maeneo haya tuwende sehemu nyingine zenye usalama zaidi tusisite kwani ni kwa usalama wetu na familia zetu" Alisema Kawaida. 





Share To:

Post A Comment: