MIILI mitano kati ya saba iliyosombwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali katika kata ya Kimochi na Mbokomu wilaya ya Moshi imeagwa leo katika viwanja vya KDC.
Mafuriko hayo yaliyotokea usiku wa kuamkia Aprili 25 mwaka huu ambapo katika miili hiyo marehemu wanne ni wa familia moja akiwamo Baba wa familia, Tito Chaki (63) pamoja na watoto wake wawili, Anjela Chaki (12), Edward Chaki (14) na mjukuu wake, Fredy Justus (6) pamoja na Jorame Kimambo (13) mkazi wa kata ya Mbokomu.
Shughuli hiyo ya kuaga miili hiyo iliongozwa na Mkuu wa wilaya ya Moshi, Zephania Sumaye, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi, Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi, Mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro, Ester Maleko, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi, Morris Makoi na wananchi na viongozi mbalimbali.
Post A Comment: