Ujenzi wa uzio waanza kwa kasi kubwa


Wananchi  wapongeza jitihada zake kwenye sekta ya Elimu


Aishukuru Serikali kwa ukarabati wa madarasa ya shule


Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini  Anthony Mavunde leo amefanya ziara kukagua ujenzi wa uzio na ukarabati wa madarasa ya Shule ya Msingi Uhuru Jijini Dodoma ambayo ni moja ya shule kongwe za Jijini Dodoma.

Mbunge Mavunde ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa marekebisho makubwa ya miundombinu ya madarasa na matundu ya vyoo kwa shule nyingi za Dodoma Jiji ikiwemo Shule ya Msingi Uhuru.

“Serikali imeleta fedha hapa kwa ajili ya ukarabati wa madarasa ya shule hii kongwe iliyojengwa mwaka 1928,kwa kuwa hali yake haikuwa ya kuridhisha ila kwa ukarabati huu itairudisha shule hii kongwe katika hali yake ya kawaida.

Na mimi kama Mbunge wa eneo hili nimeona niunge mkono jitihada za serikali kwa kuanzisha ujenzi wa uzio wa shule hii kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na kuweka mazingira mazuri ya kusoma kwa wanafunzi ambapo kwasasa eneo hili lina muingiliano mkubwa sana wa wafanyabishara na watoa huduma mbalimbali ambao shughuli zao zinaathiri wanafunzi kusoma kwa utulivu”Alisema Mavunde

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi Diwani wa Kata ya Uhuru  Khalfan Kabwe ameshukuru na kupongeza jitihada za serikali za ukarabati wa madarasi na ujenzi wa uzio unaofanywa na Mbunge wa Dodoma Mjini na kuahidi kusimamia utekelezaji wa miradi hii kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.Share To:

Post A Comment: