Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekitaka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kuendelea kusimamia Maadili ya Taifa, Kama ambavyo Muasisi wa Chuo baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere alivyosimamia uadilifu, Umoja, Upendo, na Mshikamano wakati wa Uhai wake.


Kauli hiyo imetolewa na Dkt Nchimbi wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya baba wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika Kampasi ya Kivukoni jijini Dar es Salaam ambapo pia amekitaka Chuo kuendelea kuboresha mitaala yake kwa lengo la kujenga Uadilifu Miongoni mwa Wanasiasa.


“Ni wajibu wa kila Mtanzania kuendelea kudumisha Amani, mshikamano na Umoja kwa lengo la kujenga Taifa lenye Umoja, Elimu ya kujitegemea lazima isistizwe kuanzia ngazi ya familia, lakini niseme.Kama nchi hii imewahi kupata Kiongozi aliyeaminika, na kukubalika basi ni baba wa Taifa, Mwalimu JK, Nyerere, Alisisitiza Dkt Nchimbi.


Amewataka watanzania watambue mchango wa Mwalimu Nyerere,kwa namna alivyoweza kujitoa kwa nchi yake kwa lengo la kuhakikisha Taifa linakuwa imara.

 


Akizungumza katika Kongamano hilo Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof.Shadrack Mwakalila amesema Chuo kimekuwa na kawaida ya kufanya Makongamano ya kuwaenzi Waasisi wa Taifa kwa lengo la kuendeleza Maono, Falsafa Fikra na Mawazo ya Waaaisi wa Taifa ambao ni Hayati Mwalimu JK,Nyerere na hayati Sheikh Abeid Amani Karume.


Prof. Mwakalila amesema Makongamano haya pia yanasaidia kuwaelimisha Wananchi na Vijana katikakuikumbusha Jamii historia ya nchi na Taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Chuo Mzee Stephen Wassira amemuelezea Hayati baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere alikuwa ni Muadilifu, Mwanademokrasia wa kweli, mpenda haki na usawa kwa watu aliowaongoza.

 


Kongamano hilo la siku Moja lilikuwa na MADA KUU inayosema “Mchango wa Mwalimu Nyerere katika Uongozi, Amani, Umoja na Uwajibikaji kwenye ujenzi wa Taifa” ambapo Viongozi, Wananchi na Wanafunzi walihudhuria kongamano hilo.

 

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano na Masoko,

CHUO CHA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

08.04.2024











Share To:

Post A Comment: