Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu amewataka wajumbe wa Baraza la Wafanykazi la Wizara ya afya kusimamia ubora wa huduma wakiwa katika maeneo yao.


Dkt. Jingu amesema hayo wakati akifunga Mkutano wa Baraza kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya uliofanyika Aprili 04, 2024 jijini Dodoma.

Dkt. Jingu amesema kumekua na malalamiko ya wananchi katika baadhi ya Vituo vya kutolea huduma za afya hivyo amewataka watendaji hao kusimamia vyema ubora wa huduma zitakazokidhi mahitaji ya wananchi wakihitaji huduma za afya.

"Kuna Hospitali moja ilikua inaitwa chinja chinja, nikawa najiuliza kwanini inaitwa jina hilo nikaja kugundua kuwa kulikua hakuna huduma bora zilizokua zinatolewa katika Hospitali hiyo". amesema Dkt. Jingu.

Aidha, Dkt. Jingu amewataka wajumbe hao kuwa wabunifu na kuanzisha miradi ya kimkakati itayosaidia kukuza pato la taasisi zao.

Katibu Mkuu huyo ametumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha wajumbe hao kuimarisha mawasiliano wakiwa maeneo yao ya kazi hali itakayosaidia katika kufuatilia changamoto na kuzitatua kwa uharaka pale inapohitajika.

"Tuimarishe Mawasiliano baina ya Ofisi na ofisi mtu na mtu, gonga hodi zungumza na mwenzio
muwe na vikao ili kuimarisha utendaji" amesisitiza Dkt. Jingu.

Dkt. Jingu ameongeza kuwa, kutokana na unyeti wa kazi ya sekta ya afya tija na ufasini ni vitu visivyo kwepeka.

"Sisi waahiri wetu ni wananchi, kila mmoja kwa nafasi yake asitoe mwanya kwa mwanachi kulalamikia huduma zetu, sekta ya afya athari zake zinaonekana wazi wazi tofauti na sekta zingine hivyo ni rai yangu kwenu tuimarishe umakini ili wananchi wasilalamike" amefafanua Dkt. Jingu.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Grace Magembe ametumia Mkutano huo kusema kuwa, ni aibu Mama anajifungua anaondoka na mtoto hajachanjwahii sio sawa.

"Kaeni nawatumishi, wasikilize nini wanataka, kuna mambo unashangaa ukiyasikia, kumbe lilikuwa ni tatizo la mawasiliano hii haina afya" ameonya Dkt. Magembe.

Naye Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Tumaini Nagu amesema wakiwa watoa huduma wa sekta ya Afya, hususan ni Walimu waliokaribu na maeneo ya huduma mbali ya Kufundisha lakini pia watenge muda kwa ajili yakutoa huduma ili kupunguza changamoto za kisekta" amenukuliwa Dkt. Tumaini.





Share To:

Post A Comment: