Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) siku ya tarehe 19 Februari, 2024 iliwasili Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara kwa ajili ya kuanza ziara ya kiutendaji ma Kupokelewa na Viongozi wa Chama na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Kheri James.

Aidha, Lengo la Ziara hio ni kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025, miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya 6, kukagua Uhai Chama na Jumuiya zake, kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Vijana na wananchi kwa Ujumla pamoja na kuhamaisha ushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, na kuwasihi wanachama na wananchi wote kuchagua wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa Serikari za mitaa 2024.

Katika ziara hii Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa ilifanya mambo mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo uzinduzi wa Shina la Wakereketwa la Vijana wa Bodaboda Kata ya Imboru ambapo Komredi Kawaida aliwaambia kundi hilo la Wasafirishaji Mhe. Rais Dkt. Samia anawapenda sana na ndio maana kairasimisha shughuli hiyo, pia alihasa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kufuata sheria za barabarani.

Kamati ya Utekelezaji Walitembelea mradi wa Maduka 17 wa Jumuiya ya Vijana ambapo walisikiliza na kupokea kero za Mradi huo na kuzitolea utatuzi.

Pia, walitembelea na kuzindua Shina la Wakereketwa Wafanyabiashara wa Vitunguu Katika Soko la Mazao ya Kilimo Mbulu, aidha katika Shina hilo walipokea kero mbalimbali ambazo pia ziliweza kufanyiwa kazi na kupatiwa majibu.

Mwisho, Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa walikamilisha ziara yao Wilaya ya Mbulu kwa kufanya Mkutano wa hadhara Kata ya Endamilay Wilayani Mbulu, Katika Mkutano huo Komredi Kawaida alisema mambo mengi yamefanywa na Chama Cha Mapinduzi kwa kuielekeza ma kuisimamia Serikali ya awamu ya Sita kutekeleza matakwa ya Wananchi, hata hivyo amewahakikishia kuwa Rais Dkt. Samia anawapenda na anatambua kuwa miongoni mwa watanzania anaowategemea kumuheshimisha ni pamoja na Wananchi wa Kata ya Endamilay.

Share To:

Post A Comment: