TAKRIBANI watoto 24,473 Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi wanatarajiwa kufikiwa na chanjo ya magonjwa ya Surua na Rubella, katika kipindi hiki Cha mwezi wa pili.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa utoaji wa chanjo hizo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wanatoa chanjo hiyo Kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano Kwa ajili ya kuwakingia na ugonjwa wa Surua na Rubella
“Ninachukua nafasi hii pia kuupongeza Uongozi wa Wilaya kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kuandaa shughuli hii muhimu Siku hii ni muhimu sana kwani kama nchi tunaungana na mikakati ya kidunia ya kutokomeza vifo vya watoto vinavyotokana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo”. Alisema Moyo
Moyo alisema kuwa ugonjwa wa Surua unasababishwa na Kirusi ambacho huambukizwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mtu aliyeathirika kwenda kwa mwingine.
Virusi vya Surua huweza kuathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara kiafya ikiwa ni pamoja na kutoona,kiziwi na hata kupelekea kifo na Ugonjwa huo huathiri watu wa rika zote na hauna tiba.
Moyo alisema kuwa njia kuu ya kuzuia ni kuwapatia chanjo ya Surua watoto walio chini ya miaka mitano ili waweze kupata kinga kamili dhidi ya ugonjwa wa Surua, Chanjo hutolewa mara mbili ambapo dozi ya kwanza hutolewa mara mtoto anapofikisha umri wa miezi 9 na dozi ya pili anapofikisha umri wa miezi 18 na ni muhimu mtoto akamilishe ratiba ya chanjo kama inavyotakiwa ili apate kinga kamili.
Wilaya ya Nachingwea tunatarajia kuwafikia watoto 24,473 na kwa kata ya Namatula ina jumla walengwa 550.Ni matumaini yangu makubwa kuwa lengo hili litafikiwa katika Wilaya yetu.
Moyo alimalizia kwa kuwaomba wananchi wote kujitokeza kushiriki katika Kampeni hii kwa kila mzazi au mlezi kuhakikisha watoto lengwa wanapata chanjo katika siku zilizopangwa lakini pia kuhakikisha unamtaarifu jirani,ndugu,jamaa au rafiki yoyote unaemfahamu ana mlengwa ili aweze kujua siku wahudumu watakuwa kituo gani.’’KAULI MBIU MPENDE MWANAO MPELEKE AKAPATE CHANJO”
Post A Comment: