NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Miko ana Serikali za Mitaa, Dk Festo Dugange amesema kwa mwaka 2023, wagojwa wapatao Milioni 31.2 sawa na asilimia 74 ya wagongwa wa nje walipatiwa huduma katika ngazi za afya ya msingi  huku Sh bilioni 97.9 zimekusanywa kwa mapato ya uchanguaji huduma za afya kwa mwaka 2022/23.

Dk Dugange ametoa kauli hiyo leo wakati wa kufungua mkutano wa kwanza wa mwaka wa Waganga Wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya Msingi ambao umelenga kujadili utekelezaji, mafanikio, changamoto na fursa katika utoaji wa huduma bora za afya, ustawi wa jamii na lishe kwa wananchi.

Alisema kumekuwa na mafanikio katika eneo la Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe baada ya Serikali kufanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya Afya Vifaa tiba na dawa katika awamu ya sita  chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alisema kwa mwaka 2023 jumla ya wagonjwa wan je wapatao milioni 31.2 sawa na asilimia 74 ya wagonjwa wote wan je walipata huduma katika ngazi za afya ya msingi huku Sh bilioni 97.9 zimekusanywa na kutumika katika kununua bidhaa za afya, huduma za rufaa, kuhudumia watumishi na kuimarisha miundombinu ya afya.

Aidha, Dk Dugange alisema kuanzia mwaka 2017 hadi Januari, 2024, Serikali imetumia Sh bilioni 937.2 katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya afya ambapo jumla ya vituo vya kutolewa huduma za afya 2,799 ikiwa Zahanati 1,762, Vituo vya afya 910, Hospitali za Halmashauri 127, majengo 83 ya kutolea huduma za dharura, majengo 28 kwa ajili ya wagonjwa mahututi na nyumba za watumishi 150.

Alisema katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora, Serikali imenunua na kusambaza vifaa tiba mbalimbali vyenye gharama ya Sh bilioni 364.7 zikiwemo mashine X-ray 249 na ultrasound 190 na magari 528 yenye thamani ya Sh bilioni 52, ambapo magari 316 ni ya kubebea wagonjwa na magari 212 ni ya usimamizi shirikishi.
Pia Serikali imenunua pikipiki 517 ikiwa ni hatua kubwa katika kuboresha huduma za afya, Ustawi wa Jamii na Lishe kwa wananchi.

“Tunapaswa kutambua na kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake binafsi na utashi wake wa dhati katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe na kufanya huduma bora za afya zipatikane kwa wananchi wote na kutoa kipaumbele katika sekta ya afya na huduma za jamii kwa ujumla.”

“Hii ni ishara ya dhamira thabiti ya Serikali katika kuhakikisha kuwa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe vinapewa kipaumbele cha juu. Tuendelee kumtia moyo na kumuunga mkono katika juhudi zake hizo za kizalendo, hivyo basi ni jukumu letu kuhakikisha kwamba tunaitunza na kuilinda miundombinu hii pamoja na vifaa tiba ili viweze kutoa huduma endelevu.”

Alisema pia Serikali imeweza kutoa mchango wake kwa taasisi za mashirika ya dini kupitia rasilimali fedha, watumishi na dawa ambapo kwa kupitia fedha za Mfuko wa Afya wa Pamoja kwa mwaka 2023/24 imetoa Sh bilioni 4.5 kwa hospitali 80 za mashirika ya dini zenye mikataba na Halmashauri.

Pia kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali ililipa kiasi cha Sh bilioni 57.3 ikiwa ni mishahara ya wataalam 4,993 wa afya walioajiriwa na mashirika ya dini na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano unaohitajika kuimarisha ushirikiano uliopo.

Share To:

Post A Comment: