Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo Februari 16, 2024 amekabidhi magari 13 kwa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Njombe, zoezi hilo limefanyika katika uwanja wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe zilizopo kata ya Mji Mwema Mtaa wa Lunyanywi.

Magari hayo yamekabidhiwa kwa lengo la Kwenda kutoa huduma kwa wananchi kwenye maeneo hayo ikiwa ni Pamoja na gali za kubebea wagonjwa.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri na Madereva katika hafla ya makabidhiano ya magari hayo Mhe. Mtaka amevitaka vituo ambavyo vimekabidhiwa magari hayo waende wakayatumie kwa shughuli zilizokusudiwa.

“Nakabidhi Magari haya 13 kwaajili ya kwenda kutoa huduma kwa wananchi wa mkoa wa Njombe, hivyo yatumieni Magari haya kwa malengo kusudiwa ili wananchi wapate huduma bora za matibabu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametupatia Magari haya ili tuwahudumie wananchi, na ninamshukuru Rais wetu kwa kuendelea kutupatia vitendea kazi mbalimbali kwenye sekta mbalimbali kwenye mkoa wetu ikiwa ni Pamoja na Idara ya Afya.”amesema Mhe. Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Share To:

Post A Comment: