Na Dickson Mnzava Same.

Kamishina wa uhifadhi wakala wa huduma za misitu Tanzania prof.DOS SANTOS SILAYO ameshiriki kwenye zoezi la upandaji miti kwenye shule ya msingi Same iliyopo wilayani Same Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kuelekea siku ya upandaji miti duniani March 21.

Akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti kwenye shule hiyo Prof.Silayo amewataka wananchi kuwa na dhana ya upandaji miti ya aina mbalimbali kwenye maeneo yao ili kuendelea kutunza mazingira.

Amesema misitu ni uti wa mgongo katika maendeleo ya sekta nyingi hapa Nchini na duniani kwaujumla hivyo kwakulitambua hilo serikali ya Tanzania imekuwa kipaumbele katika utunzaji wa mazingira

."katika maendeleo ya Taifa lolote lile duniani hutegemea miti kwani misitu pekee huzalisha malighafi nyingi sambamba na hewa ya oksijeni ambayo hutumiwa na kila mwanadam yeyote aliye hai duniani hivyo utunzaji wa mazingira kwetu kama Taifa ni kipaumbele namba moja katika kutetea maisha ya viumbe hai ikiwa ni pamoja na binadam"Alisema Prof.Silayo

Balozi wa mazingira Nchini Ahidi Sinene amesema katika dunia ya sasa vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika upandaji wa miti kwani hali ya mazingira kwasasa sio nzuri na vijana wasipokuwa mstari wa mbele kupambana na swala hili basi Taifa linalokuja litakuwa katika wakati mgumu sana.






 

Share To:

ASHRACK

Post A Comment: