Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani litaanza ukaguzi wa magari kutumia Tehama sanjari na Mitambo Mizito na Teknolojia ya IHET badala ya ukaguzi wa kutumia ramli kuanzia Machi mwaka huu.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini,Ramadhani Ng’anzi alisema kuanzia mwezi Machi mwaka huu jeshi hilo litaanza kazi ya ukaguzi wa magari kwa kutumia vifaa vya kisasa zaidi.
 
Alisema mafunzo ya wakaguzi wa magari yanalengo la kuhakikisha kaguzi za magari zitakuwa pana zaidi ikiwemo uwepo wa barabara salama katika kupunguza ajali za barabarani.
 
“Tutaanza kukagua magari kwa kutumia mitambo maalum nanmsimu huu tutaanza rasmi kukagua magari kwa kutumia mitambo ya kisasa na badaye taarifa za kaguzi za magari hayo zitaingia kwenye mfumo data,tutaachana na ukaguzi wa kupiga ramli”
 
Naye Johansen Kahatano ambaye ni Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara kutoka LATRA  alikipongeza Chuo Cha Ufundi Arusha (ATC) kwakutoa mafunzo sahihi ya udereva sanjari na utoaji huduma kwa wananchi wakiwemo abiria pale zinapotokeq dharura barabarani lakini pia alitoa rai kwa madereva kuhakikisha wanatumia vyuo sahihi vya udereva ili kupunguza ajali za barabarani sanjari na kuhakikisha magari yao yanakaguliwa ili kuwezesha ubora.
 
Huku Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Arusha (ATC) Profesa, Musa Chacha alishukuru mafunzo hayo ya siku mbili kufanyika chuoni hapo ili kuongeza ujuzi zaidi katika kupunguza ajali barabarani kwa kutoka mafunzo bora kwa madereva ili kutoka huduma za usafiri kwa uadilifu ikiwemo kutoa mbinu za muda sahihi za kuendesha gari na njia za kutoa kwa madereva
 
Lakini pia alisema mfumo huo utatoa taarifa sahihi za udhibiti  wa shule za udereva nchini ili kupata wataalam wa fani waliopata mafunzo katika vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
 
Awali Kiongozi wa Madereva wanaotoa huduma kwenye magari  ya utalii Timoth Abel alipongeza ushirikiano wanaopata kutoka kikosi cha usalama barabarani haswa katika kaguzi za magari hayo na kuomba vituo zaidi kuongezwa vya ukaguzi ili kupunguza muda wa watalii au wageni wengine kukaa muda mrefu kwaaajili ya kaguzi.
Share To:

Post A Comment: