Benki ya NMB imekabidhi madawati na Vifaa vya ujenzi kwa shule Tano( 5) katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoani mara pamoja na ukarabati wa majengo Katika shule ya Msingi minigo vikigharimu kiasi cha shilingi Milion 84.
Akikabidhi madawati hayo Kaimu Meneja wa benki hiyo kanda ya ziwa Hamadan Silliah amesema utoaji wa Vifaa hivyo kwa shule nikarejesha shukrani kwa jamii wanayoihudumia katika maeneo mbalimbali hapa Nchini
Amesema NMB imekuwa ikipokea maombi mbalimbali kutoka katika taasisi ambapo nao wamekuwa wepesi kuitika kusaidia ilikuhakikisha wanaiunga Mkono Serikali katika utekelezaji wa Maendeleo hapa Nchini.
“hapa Leo tunakabidhi Vifaa vyenye thamani ya Milioni 84 lengo nikuisaidia serikali nikuboresha sekta ya Elimu hapa Nchini lakini pia tumekuwa tukitoa msaada hata kwenye majanga mbalimbali” Hamadan Silliah Kaimu meneja NMB kanda ya ziwa.
Akipokea msaada huo mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Issa Chikoka ameishukuru benki hiyo huku akiwaomba pia kuwekeza nguvu zao katika sekta ya kilimo na uvuvi kwani asilimia 77 Wilaya ya Rorya inazungukwa na Ziwa Victoria.
Baadhi ya wanafunzi na walimu wamesema msaada huo wa madawati utakuwa chachu katika kupiga hatua nakuondokana na kadhia ya wanafunzi kugombani Dawati na wengine kukaa chini hali ilivyokuwa ikishisha molari wawanafunzi hao kuhudhuria masomo.
Post A Comment: