Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko amewaelekeza Wakuu wa Mikoa wote Nchini pamoja Wakuu wa wilaya kusimamia vyema utekelezaji huduma ya mama na mtoto kwa kuwaunganisha wadau na wananchi katika kuokoa Maisha ya mama na mtoto.


Dkt Biteko ameyasema hayo Leo machi 25,2024 Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Afya msingi Nchini uliohudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi pamoja na Waganga wakuu wa Mikoa na Waganga wakuu wafawidhi wa hospital za halmashauri.

Katika hilo Dkt Biteko ametoa wito kwa wananchi wote kuitumia namba hii kwa kuipiga inapotokea dharula ili kuokoa vifo vya mama na mtoto.

"Nitumie nafasi hii kuwaelekeza wakuu wa mkoa wote Nchini pamoja na wakuu wa wilaya kusimamia vyema utekelezaji wa huduma kwa mama na mtoto kuwafanya wadau na wananchi wote kuwa sehemu ya kuokoa vifo vya mama na mtoto".

"Ninayo furaha kubwa sana kuzindua huduma hii ya mama na mtoto ya mama. Hivyo wito wangu kwa wananchi wote wakike na kiume kutumia namba hii kuwasiliana pale inapotokea dharula ili tusikubali kupoteza maisha ya mama zetu na watoto wetu na hii namba itaendelea kutoa huduma wakati wote"

Aidha Naibu Waziri Mkuu amezitaka Wizara zinazohusika na sekta ya Afya uwekezaji wa miundombinu iliyowekwa na Serikali katika vituo vya afya msingi inatunzwa.

"Niseme kuwa Wizara zinazohusika na sekta ya afya wekeni mpango wa kuhakikisha kuwa uwekezaji wa miundombinu uliofanywa na Serikali katika vituo vya afya msingi inatunzwa,haina maana yeyote kituo kimejengwa leo na baada ya muda kimeharibika miundombinu itunzwe".

Akitoa salamu za wizara ya Afya kwaniaba ya Waziri wa afya Naibu Waziri wa afya Dkt Godwin Mollel amesema kuwa afya ni uchumi kwani bila afya hakuna kitu kitakachosonga mbele mfano upo hata kipindi cha króna hakuna kitu chochote kilichofanyika ikiwemo veranda.

"Ndomana tunasema afya ni uchumi katika kipindi cha korona hakuna kilichoweza kuendelea,hakuna kiwanda kilichofanya kazi,hakuna shughuli yeyote ya kiuchumi iliyosonga mbele na shughuli za kiuchumi zilisimama,manake ukigusa eneo la afya na watu wa afya wakasimama katika nafasi zao basi unaboreshs uchumi".

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya afya na lishe Dkt Festo Dugange amesema kuwa hadi February 2024 sekta ya afya msingi nchini Tanzania ina jumla ya vituo vya kutea huduma za afya 6,933 zikiwemo Zahanati, na Hospitali za Halmashauri ukilinganisha na mwaka 2015 ambapo idadi ilikuwa ni 5,270.

"Kufikia February 2024 sekta ya afya msingi Nchini Tanzania ina jumla ya vituo vya kutolea huduma ya afya 6,933 zikiwemo Zahanati 5,887 vituo vya afya 874 na hospital za halmashauri 172. Takwimu hizi zinaonesha kwamba kuna ongezeko kubwa la vituo katika afya msingi ikilinganishwa na idadi ya vituo 5,270 katika mwaka 2015. Hii ni hatua kubwa katika kuendelea kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wote nchini Tanzania".

Aidha Dkt Dugange ameongeza kwa kutoa idadi ya wateja wa nje (OPD)na wateja wa ndani (IPD) kwa mwaka 2023 waliopata huduma katika vituo vya afya.

"Aidha kwa mwaka 2023 wateja milioni 26.9 walipata huduma katika vituo vya afya msingi kama wagonjwa wa nje yani (OPD) wateja 854,318 walipata huduma ya kulazwa (IPD). Katika eneo la mama na mtoto jumla ya wateja milioni 1.6 walijifungulia katika vituo vya kutolea huduma afya msingi na wakina mama waliokuwa na uzazi pingamizi wakafanyia upasuaji walikuwa ni 125,318".

Kuanzia mwaka 2017 hadi January 2024 hospital za halmashauri zimeongezeka kutoka hospital 50 mpaka kufikia hospital 177.






Share To:

Post A Comment: