Na Edwin Lamtey ; Hai
Mwili wa mwanamke anayesadikika kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 40 umeokotwa ukiwa umeoza na  kutelekezwa pembezoni mwa barabara ya Moshi Arusha karibu na eneo la Kwa Wasomali kitongoji cha Darajani kijiji cha Sanya Station wilayani Hai.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kitongoji cha Darajani kijiji cha Sanya Station Rabson Mmbasha amesema kuwa alipigiwa simu na balozi wa eneo hilo akidai kuwa kuna mwili umeonekana katika eneo hilo.

“Ni usiku wa tarehe 27 kuamkia 28 majira ya saa nne nilipigiwa simu na balozi wangu kunieleza hili tukio na mimi niliwasiliana na polisi Bomang’ombe na kisha walikuja maaskari wakauona mwili kisha wakasema tuuache tutawanyike hadi kesho asubuhi (leo) ambapo wamekuja wakiwa na daktari na baada ya kuchukua taarifa”. Alisema Bw. Mbasha

Kufuatia mwili huo kuoza na kuanza kutoa harufu jeshi la polisi liliamuru mwili huo kuzikwa katika eneo la pembezoni mwa barabara hiyo ambapo ni eneo la hifadhi ya barabara linalomilikiwa na TANROAD.

Alipotafutwa kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amesema kuwa hana taarifa hiyo na kuahidi kuwasiliana na OCD wilaya ya Hai kwa ajili ya ufuatiliaji na kupata taarifa kamili.

Share To:

Post A Comment: