Dickson Mnzava, Same.

Halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro imekabidhi pikipiki 7 kwa maafisa Organ Kutoka kwenye Kata 7 ndani ya Wilaya hiyo.

Akizungumza 29 /01/2024 wakati akikabidhi pikipiki hizo mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Same Yusto Mapande amewataka maafisa Organ hao kutumia vyombo hivyo katika kuwapatia wananchi huduma ili wananchi waweze kuona mafanikio ya serikali yao.

Mapande amesema wapo baadhi ya watendaji wa serikali ambao sio waadilifu na wanapopewa vyombo hivyo hugeuza matumizi yake na kufanya vyombo hivyo kuwa sehemu ya wao kujipatia kipato kitu ambacho ni kinyume na maadili ya kazi.

Amewataka maafisa Organ hao kwenda kuhudumia wananchi kwausawa na kwauadilifu pasipo kujitokeza malalamiko yeyote na wananchi wafurahie matunda ya serikali yao.
“Tunawapa vyombo hivi hapa leo naomba nendeni kutoa huduma iliyobora kwa wananchi wetu tusifanye matumizi mabaya ya mali hizi za serikali mpatiwa kwa lengo mahususi la kutoa huduma kwa wananchi wetu na si vingine oneni sasa namna ya kukutana na wafugaji na kuwasaidia”
“Alisema Mapande”

Afisa Kilimo, mifugo na uvuvi wilayani Same Cainan Kiswaga amesema kulingana na jografia ya maeneo mengi ya Wilaya hiyo ya Same kuwa na changamoto kubwa ya kufikika kitu ambacho hurorotesha utoaji huduma kwa wananchi kwa wakati uwepo wa pikipiki hizo utaongeza nguvu zaidi ya ufanisi kazini kwa watumishi hao.

Kiswaga ameishukuru serikali ya awamu ya sita kwakuona na kusikiliza kilio cha watumishi hao akiwataka maafisa Organ hao kwenda kutimiza yote kwa vitendo.

Nao baadhi ya maafisa Organ hao akiwemo Evarest Masawe Afisa organ Kutoka Kata ya Ndungu na Ambisile Myale Kutoka Kata ya Mabilioni wamesema uwepo wa pikipiki hizo sasa utasaidia kuondoa malalamiko kwa wafugaji kwani watakuwa wanawafikia kwa wakati na kutoa huduma.

Share To:

Post A Comment: